Cart 0
Si amini kuwa ni mimi! (Swahili)

Si amini kuwa ni mimi! (Swahili)

$0.00

NI JAMBO LA ajabu tuwezavyo kuona wazi nyuso za watu wengine kumbe nyuso zetu wenyewe hatuwezi kuziona. Kioo chatusaidia kuona haya yote. Kwa kutumia kioo twaweza kujiona vizuri wenyewe. Kinatusaidia kuona ambacho kimekaa si sawa tuweze kukifanya na kuwa sawa.

Kioo chatuonyesha hali ya nnje jinsi tulivyo. Kuna kioo ambacho chatuonyesha hali ya ndani jinsi tulivyo. Kioo hiki ni cha namna gani? Ni Biblia.

Yule ambaye si Mkristo akisoma Biblia au kusikia Biblia jinsi ifundishavyo ataona mfano wa moyo wake: ‘Hasira, Uovu, Machukizo, Uwongo.’ Wakolossai 3:8-9. ‘Ukafiri, Tamaa, Mawazo mabaya, kwa ajili ya hayo ghadhabu ya Mungu huwafikia wana waasi.’ ‘Pasipo Kristo hakuna tumaini, hakuna Mungu duniani.’ Waefeso 2:12.

Unasema, ‘Huamini kuwa ni wewe? Kama hujawa Mkristo fahamukiwa kwamba ni sanamu ya kweli ya moyo wako. Kioo cha sema kweli. Mawazo yako yasema, ‘Ndio hii ni kweli yangu.’

Lakini tukiwatumekwisha simama mbele ya kioo nakuona jinsi mioyo yetu ilivyo, ndivyo Biblia itakavyo tufanya tuweze kusimama mbele za mtu. Ana upendo, busara, na nguvu. Asema nasi, ‘Natambua moyo wako ni mdhaifu, lakini naweza kuuponya. Nafahamu moyo wako mchafu naweza kuufanya kuwa safi. Nafahamu umekosa, lakini nimekufa kwa ajili yako upate kusamehewa. Njoo kwangu. ‘Nitakupokea na kukulinda.’

Yesu atanisamehe: ‘Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu.’ I Yohana 1:9

Atakusafisha moyo wako: ‘Damu ya Yesu Kristo yatusafisha kutoka katika dhambi zote.’ Yohana wa 1, 1:7.

Atakupa nguvu: ‘Nayaweza mambo yote katika Kristo anitiaye nguvu.’ Wafilipi 4:13.

Atakupa amani: ‘Bwana wa amani mwenyewe na awape amani daima.’ 11 Wathesolonike 3:16.

Atakupa furaha: ‘Ili furaha yangu iwe ndani yenu na furaha yenu itimizwe.’ Yohana 15:11. Hakuna yeyote awezae kukutendea mengi kama Bwana Yesu Kristo. Mkubali aingie moyoni mwako.

Ahsante Mungu Kwa Biblia
Yatutambulisha Uovu Wa Mioyo Yetu
Yatutambulisha Yule Awezae Kufanya Kila Kitu Kwa Haki
Bwana Yesu Kristo
Je Ni Bwana Wako Ba Mwokozi?More from this collection