Cart 0
Ni Nani  Aliyemsulubisha Kristo? (Swahili)

Ni Nani Aliyemsulubisha Kristo? (Swahili)

$0.00

JE, NI WARUMI? NDIYO KWA NJIA FULANI
“Pilato akipenda kuwaridhisha makutano, akawafungulia Baraba; akamtoa Yesu, baada ya kumpiga mijeledi, ili asulibiwe” (Marko 15:15).

JE, NI WAYAHUDI? NDIYO KWA NJIA FULANI
“Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua” (Mathayo 26:59).

JE, Nl YUDA ISKARIOTE? NDIYO KWA NJIA FULANI
“Yuda Iskariote, yule mmoja katika wale thenashara, akaenda zake kwa wakuu wa makuhani, apate kumsaliti kwao” (Marko 14:10). “Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyo-andikiwa; lakini ole wake mtu yule ambaye amsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu yule kama asingalizaliwa” (Mathayo 26:24).

JE, NI MUNGU? NDIYO KWA NJIA FULANI
“Hakika ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu; lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, amepigwa na Mungu, na kuteswa” (Isaya 53:4). “Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?” (Warumi 8:32).

JE, NI WEWE? NDIYO, HILI NDILO JIBU KAMILI
“Na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote” (Isaya 53:6) . “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo ali-kufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi”(Warumi 5:8). “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona” (Isaya 53:5). “Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi” (1 Timotheo 1:15).

OH UPENDO WA MUNGU
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu” (1 Petero 3:18).

JE, UTATHUBUTU KUUKATA UPENDO HUU?
“Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia” (Yohana 3:36). “Sisi je! tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii?” (Waebrania 2:3).More from this collection