Cart 0
Manemo Manne Yenye Maana (Swahili)

Manemo Manne Yenye Maana (Swahili)

$0.00

1. Jinsi Dhambi Ilivyo.
Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu. I Yohana 1:8. Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; hakuna amtafutyaye Mungu… Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Warumi 3:10, 11, 23. Kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote wa sababu wote wamefanya rhombi. Warumi 5:12. Ile dhambi ikiisha kukomaa huzza mauti. Yakobo 1:15.

2: Jinsi Mungu Apendavyo Binadamu.
Kwa magna jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hate akamtoa Mwanawe pewee, ili kila mtu amwamiluye asipotee, bali awe na uzima wa milde. Yohana 3:16. Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amentuma Mwanawe pewee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye. Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zeta. I Yohana 4:9-10.

3. Msalaba Wa Kristo.
Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye. Yohana 3:14-15. Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye rhombi. Warumi 5:8. Kwa maana Kristo naye aliteswa mare moja kwa ajili ya dhambi, mwenye hski kwa ajili yao wasio kaki, ili atulete kwa Mungu. I Petro 3:18. Kristo Yesu… alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya woke. I Timotheo 2:6.

4. Jinsi Kristo Awezavyo Kuokoa Mwenye Dhambi.
Yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? …Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka. Matendo 16:30-31. Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jinging chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo. Matendo 4:12. Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamhlia. Yohana 3:36. Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Warumi 10:13.

HAYA, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani. Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono. Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milde, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.

Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa kabila za watu. Tazama, utaita taifa usilolijua, na taiga lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya Bwana, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.

Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. Isaya 55:1-7.More from this collection